![]() | Wakati: Mizingo na Vitu Vinavyojirudia |
Mara nyingine unataka kuiambia kompyuta kurudia kitu mara nyingine na nyingine tena. Mzingo hutumika kuifanya kompyuta kufanya kitu zaidi ya mara moja.
Aina mojawapo ya mzingo ni mzingo usio na mwisho. Kwa mzingo usiomwisho kompyuta hufanya amri hiyo hiyo tena na tena. Kompyuta itaendelea kurudia amri hiyo milele.
Unatengeneza mzingo usio na mwisho kwa agizo la "wakati(kweli)". Kwanza, unaandika wakati(kweli). Baada ya hapo weka bano mawimbi la kufungua. Kisha, weka maagizo yote ambayo unataka kompyuta kurudia. Mwishoni, weka bano mawimbi la kufunga. Kwa mfano, kwenye programu hapo juu, kompyuta itakuwa ikikwambia ni jinsi gani ulivyo Mkuu na jinsi inavyokupenda.
Kompyuta itaendelea tu kurudia maagizo kutoka kwenye mzingo usio na mwisho milele. Kuifanya kompyuta kuacha utatakiwa kubonyeza kitufe cha simama.
Mizingo ina manufaa katika kuhesabu vitu. Programu hapo juu inaanzia moja na kuendelea kuhesabu. Kumbuka kubonyeza kitufe cha simama unapotaka kompyuta kuacha.
Mwanzoni, n ni 1. Kompyuta inakuonesha hili. Kisha, inaongeza 1 kwa n, kupata 2. Na kisha, inaonesha 2 kwenye skrini. Kisha, inaongeza 1 tena kwa n, kupata 3. Na inaonesha hili kwenye skrini. Na hii inaendelea tena na tena. Kwa kufanya hivi, kompyuta inaweza kuhesabu namba.
Aghalabu, hutotaka kompyuta kurudia kitu milele. Kwenye Babylscript, kuna agizo linaitwa "vunja". Kompyuta inapoona agizo la vunja, inasimama kurudia vitu.
Programu hii inatumia agizo la vunja kuhesabu kuanzia 1 mpaka 5. n inaanza na 1. Kila mara mzingo unaporudia, n huongezeka kwa 1. Lakini n inapokuwa 5, mzingo husimama, na kompyuta husema "Imekamilika".
Unaweza pia kutumia vunja kusimamisha mzingo pale kitu fulani muhimu kinapotokea. Kwenye programu hii, kompyuta hukuuliza swali. Itaendelea kukuuliza swali hilo hilo hadi utakapotoa jibu sahihi.
Kushoto, unatakiwa kuandika programu ya kurusha roketi. Kurusha roketi, unatakiwa kwanza uhesabu kwenda chini kuanzia 30 mpaka 1. Kuna mashine ya kuhesabia. Unaweza kuipa "mashine" agizo la "sema" pamoja na naumba ya kuhesabu. Unatakiwa kuifanya mashine iseme namba kuanzia 30 kwenda chini mpaka 1. Baada ya hapo, utoa agizo la "nyanyuka" kwa mashine. Kama namba zilihesabiwa kwa usahihi, roketi itaruka angani. Tumia mzingo kuhesabu. Kodi yako itafanana na kodi ya kuhesabu kutoka 1 mpaka 5.