KuanzaKutoa Amri kwa VituProgramu 1Programu 2KikokotoziVibadilikavyo: Kukumbuka VituMitungo 1Mitungo 2IngizoIkiwaWakati: Mizingo na Vitu VinavyojirudiaNamba Nasibu na ChaguaFSM: Mashine ya Hali Yenye Kikomo
Kuanza

Kompyuta hazina werevu sana. Kweli, zinaweza kufanya hesabu nyingi au kukusaidia kutafuta taarifa kwenye wavuti. Lakini, kama ungeiambia kompyuta kusafisha nyumba kwa ajili yako, Je ingeweza kufanya? Kama ungeiambia kompyuta ikuchoree picha ya ndege, ingefanya? Kompyuta isingekuwa na habari kuhusu kitu unachokisema.

Uelewa wa kompyuta ni mdogo. Kama hutozipa maelekezo kamili, zinachanganyikiwa na kufanya makosa. Kuiambia kompyuta ni kitu gani unataka ifanye wakati mwingine ni vigumu kwa sababu unatakiwa kuelezea vitu kwa umakini.

Kwa kuwa kompyuta hazielewi Kiswahili, unatakiwa kutoa maelekezo katika lugha maalum za kompyuta ambazo kompyuta zitaweza kuelewa. Tovuti hii itakufundisha lugha ya Babylscript, lugha yenye asili ya lugha ya JavaScript. Kompyuta nyingi zinaelewa lugha ya JavaScript.

Usivunjike moyo kama utandika Babylscript ambayo kompyuta haielewi. Kumbuka kwamba kompyuta ni nyepesi kuchanganyikiwa, na maelekezo yote ya Babylscript yanatakiwa kuwa sahihi na kamili. Kompyuta huchagua sana! Matatizo au makosa madogo kwenye Babylscript huitwa kunguni. Hata waandika programu wazuri kabisa hutengeneza kunguni wengi, wengi sana.

Programming Basics

Programming Basics: Beginners

Barua Pepe | Kuhusu | Sera ya Faragha