Tvbot alitembelea mwezi hivi karibuni. Kuna mashimo na milima mingi mwezini, na Tvbot alipotea. Tvbot anahitaji msaada wako kurudi kwenye meli yake.
Kushoto, unaweza kumwona Tvbot mwezini. Unaweza kumtembeza Tvbot kwa kutumia amri za "juu", "chini", "kushoto" na "kulia".
Tvbot hawezi kwenda nje ya mstari wa kijani. Tvbot atasubiri tu kama hataweza kufuata amri yako.
Toa maelekezo kwa Tvbot kuhusu jinsi ya kurudi kwenye meli yake. Tvbot anatakiwa afike kwenye eneo la bluu ili kuingia kwenye meli.