Mpaka sasa, umekuwa ukifanyakazi sanasana na namba kwenye programu zako. Kama unataka kutumia maneno kwenye programu, unahitaji kitu kinachoitwa Mtungo.
Mtungo ni kitita cha herufi au maneno ndani ya alama za dondoo. Unaweza kuwa na alama (isipokuwa kwa \ na ") na namba ndani ya alama za dondoo pia. Ukijaribu kuonesha mtungo, kila kitu isipokuwa alama za dondoo kitaoneshwa.
Ni muhimu kuwa na alama za dondoo mwanzoni na mwishoni mwa mtungo. Kompyuta si erevu sana na zinaweza kuchanganyikiwa kirahisi. Itafikiri unajaribu kutumia kibadilikacho!
Kushoto, kuna Eneo la Kuprogramu ambapo unaweza kujaribu kuonesha mitungo tofauti kwenye skrini. Pia kuna roboti maalum aitwaye botmtendaji ambaye anaweza kufanya matendo flaniflani. Kitu botmtendaji kinaelewa amri ya sema. Kama ukimpa botmtendaji mtungo wa kusema, botmtendaji atausema. Unaweza pia kumfanya botmtendaji aseme namba.
Mitungo inaweza kuwekwa kwenye vibadilikavyo kama namba tu.
Tofauti na namba, huwezi kufanya hesabu na mitungo. Ukijaribu kujumlisha mitungo pamoja, mitungo hiyo miwili itaunganishwa pamoja. Kuwa makini unapokuwa na namba ndani ya mtungo! Unapozijumilisha pamoja, mitungo hiyo miwili inaunganishwa na siyo kujumlishwa.