KuanzaKutoa Amri kwa VituProgramu 1Programu 2KikokotoziVibadilikavyo: Kukumbuka VituMitungo 1Mitungo 2IngizoIkiwaWakati: Mizingo na Vitu VinavyojirudiaNamba Nasibu na ChaguaFSM: Mashine ya Hali Yenye Kikomo
FSM: Mashine ya Hali Yenye Kikomo

Mashine ya Hali Yenye Kikomo siyo mashine flani ya kijinga. Mashine ya Hali Yenye Kikomo ni njia mojawapo ya kuandika programu. Mashine ya Hali Yenye Kikomo kwa kawaida huitwa FSM (Finite State Mashine).

FSM inaundwa na vitu viwili. Kwanza, ina maandishi kuhusu nini kinatokea. Kisha, ina mishale ya kukuonesha chaguzi tofauti unazoweza kufanya. Unatakiwa ufanye uchaguzi na kufuata mshale.

FSM ni nzuri kutengenezea michezo na hadithi. Hapa ni mchezo ambao unatakiwa kutafuta hazina. Kwanza, nenda Mwanzo. Kisha, fuata mishale mpaka utakapofika mwisho.

Hii ni FSM rahisi ambayo inakufanya uweze kutafiti chumba.

Tujaribu kutengeneza program ambayo utakufanya uweze kutafiti chumba. Kwanza, toa namba kwa vyumba vyote.

Sasa tutaanza kuprogramu. Wakati wa kuprogramu FSM, unataka kompyuta kujua ni chumba gani upo. Unatakiwa uanze na chumba namba 1.

Kompyuta itakuambia mambo tofauti ikitegemea uko chumba gani.

Kompyuta itakuuliza pia wapi unataka kwenda. Kompyuta kisha itabadilisha namba ya chumba kutokana na jibu lako.

Baada ya chumba chako kubadilika, kompyuta itatakiwa kurudi mwanzo na kukwambia kuhusu chumba kipya. Unaweza kutumia mzingo kwa hili.

Ni hivyo tu! Unaweza kuendesha programu sasa. Utaweza kutembelea vyumba tofauti.

Jaribu kuchukua FSM ya mchezo wa hazina na kuiprogramu kwenye kompyuta. Kisha, jaribu kutengeneza mchezo wako mwenyewe wa FSM.

Programming Basics

Programming Basics: Beginners

Barua Pepe | Kuhusu | Sera ya Faragha