Unaweza kutumia Babylscript kufanya hesabu kama ni kikokotozi.
Kumbuka unaweza kutumia amri ya "onesha" kuonesha namba kwenye skrini.
Unaweza kujumlisha namba kwa kuandika namba mbili na kuweka alama ya jumlisha katikati yazo. Endelea na ujaribu kushoto.
Unaweza kufanya aina nyingine za hesabu kwa kutumia alama tofauti. Kwa kuwa hakuna vitufe vya "zidisha" au "gawanya" kwenye baobonye, unatakiwa kutumia * au / badala yake.
Unaweza pia kuweka hesabu nyingi kwenye mstari mmoja na kufanya mahesabu yote kwenye mstari huo huo.
Unatakiwa kuwa makini hata. Babylscript haifanyi hesabu kutoka kushoto kwenda kulia. Inatumia utaratibu maalum wa kihesabu.