KuanzaKutoa Amri kwa VituProgramu 1Programu 2KikokotoziVibadilikavyo: Kukumbuka VituMitungo 1Mitungo 2IngizoIkiwaWakati: Mizingo na Vitu VinavyojirudiaNamba Nasibu na ChaguaFSM: Mashine ya Hali Yenye Kikomo
Vibadilikavyo: Kukumbuka Vitu

Kompyuta ina kumbukumbu na inaweza kukumbuka vitu. Kuifanya kompyuta ikumbuke vitu, unatumia vibadilikavyo. Kibadilikacho ni kipande cha taarifa kikiwa na jina la taarifa hiyo.

Tuseme unanunua vitu vya nyumbani, na unahitaji kununua matufaha matano. Unaweza kuiambia kompyuta ikumbuke ni matufaha mangapi unahitaji kununua. Unaweza kutumia kibadilikacho kwa hili.

Kwenye Eneo la Kuprogramu la bluu, andika "matufaha=5;"

Unapoendesha programu, kompyuta sasa itahifadhi namba 5 kwenye kumbukumbu yake. Itakipa kipande hicho cha taarifa jina "matufaha".

Kupata taarifa kutoka kwenye kompyuta, unaiambia tu kompyuta jina la taarifa unayoitafuta. Kompyuta itaangalia kwenye kumbukumbu yake kupata hiyo taarifa na kukupa.

Mwisho wa programu, andika "onesha(matufaha);" Utakapoendesha programu, kompyuta itaona kwamba matufaha ni kibadilikacho. Itaangalia kwenye kumbukumbu yake na kukuonesha kwamba imekumbuka kwamba uliweka 5 pale mwanzoni kwenye programu.

Vibadilikavyo vinaweza kupewa jina lolote ambalo halina alama yoyote ya ajabu. Jina la kibadilikacho linaweza kuwa na namba ndani yake ilimradi jina hilo halianzi na namba. Hapa, tuna orodha ya vitu vya nyumbani tunavyotakiwa kununua.

Hakikisha unaandika kibadilikacho namna ile ile kila mara. Na hakikisha huchanganyi herufi kubwa na ndogo! Kama utatumia kibadilikacho ambacho kompyuta haikijui, au utaandika kibadilikacho vibaya, kompyuta italalamika.

Unaweza kutumia vibadilikavyo kwenye hesabu. Kwa mfano, badala ya kutumia "onesha(2+4);" unaweza kutumia "onesha(saladi + figili);" Vyote ni sawa. Jaribu.

Unaweza pia kufanya hesabu na kuweka vyote katika kibadilikacho. Unaweza hata kutumia vibadilikavyo kwenye hesabu. Angalia hapa njia tatu tofauti za kuweka vitu kwenye kibadilikacho mboga. Vyote ni sawa.

Chukulia kwamba rafiki yako anataka kuoka kitobosha cha tufaha na anakuomba ununue matufaha mawili zaidi. Kufanya hivyo, unaweza tu kuchukua kiasi cha zamani cha matufaha ambacho ulitaka na kuongeza mbili kwake. Hivyo orodha yako ya vitu vya nyumbani itakuwa na matufaha mawili zaidi.

Kitu kimoja cha ajabu cha vibadilikavyo ni kwamba kompyuta husahau kila kitu kila mara programu inapoendeshwa. Kwa hiyo mwanzo wa programu, unatakiwa upange vibadilikavyo vyote tena.

|

Programming Basics

Programming Basics: Beginners

Barua Pepe | Kuhusu | Sera ya Faragha