![]() | Ikiwa |
Programu huiacha kompyuta kufuata maagizo, lakini mpaka sasa kompyuta haijui kufanya maamuzi.
Kwa agizo la "ikiwa", kompyuta inaweza kulinganisha vitu viwili na kufanya maamuzi. Njia moja kompyuta inaweza kulinganisha vitu ni kuangalia kama vitu viwili ni sawa.
Unaweza kufanya hivi kwa kuandika "ikiwa" ikifuatia na bano la kufungua "(". Kisha unaandika kitu cha kwanza unataka kompyuta kukiangalia. Kisha unaandika alama mbili za sawasawa na kisha kitu cha pili unataka kompyuta kukiangalia. Baada ya hapo, unaandika bano la kufunga ")", na kisha bano la kufungua lenye mawimbi "{". Kisha unaipa kompyuta maagizo ambayo itafuata kama vitu hivyo viwili NI sawa. Kisha unaandika bano la kufunga lenye mawimbi "}".
Kwenye programu hii ndogo, ikiwa utajibu ndiyo, kompyuta itakuambia ulete mwamvuli. Kama utaandika kitu ambacho siyo sawa na "ndiyo" basi kompyuta haitafanya chochote. Unaweza kuandika "hapana" au "hainyeshi" na kompyuta haitafanya chochote. Ikiwa utatumia herufi nyingine kama "nDiYo", siyo sawa kabisa na "ndiyo" na kompyuta haitafanya chochote pia.
Alama ya mshangao ikifuatiwa na alama ya sawasawa inamaanisha "siyo sawa". Kwenye programu hapo juu, kompyuta inaangalia kwanza kama uliandika "ndiyo". Ikiwa ni hivyo, itakuambia ulete mwamvuli. Kisha itaangalia kama uliandika kitu kingine tofauti na "ndiyo". Ikiwa hivyo, itakuambia uvae miwani ya jua badala yake.
Badala ya kuwa na maagizo mawili tofauti ya ikiwa, unaweza kutumia agizo la lasivyo. Kwenye programu hapo juu, ikiwa a ni ndiyo basi itafanya kitu kimoja. Ikiwa a siyo "ndiyo" basi itafanya maagizo yanayofuata baada ya lasivyo. Kisha ona kwamba unaweza kuwa na agizo zaidi ya moja ndani ya mabano yenye mawimbi. Na unaweza kuweka vitu kwenye mistari tofauti ili kufanya vitu rahisi kusoma.
Hii ina manufaa kwa sababu unaweza kuwa na maagizo mengi ya ikiwa yote yakiwekwa pamoja. Hapa, ikiwa utaandika "jua", "mvua", au "baridi" kompyuta itakuambia nini cha kuvaa. Ikiwa utaandika kitu kingine, kompyuta itaenda moja kwa moja mpaka mwisho na kukuambia haielewi ulichoandika.
Kushoto, unatakiwa kuandika programu ya mashine ya kuchanganya rangi. Inatumia rangi nyekundu, bluu, na njano kutengeneza aina nyingine za rangi.
Amri mashine.agizo() inauliza ni rangi gani kutengenezwa. Kisha inakupa mtungo wenye jina la rangi. Unatakiwa kuifanya mashine itengeneze rangi ya aina hiyo. Kwanza, unatakiwa kutumia mashine.kichukuzi(), kusogeza ndoo ya rangi chini ya vinyunyizio kwenye mkanda wa kichukuzi. nyekundu.nyunyizia(), bluu.nyunyizia(), na njano.nyunyizia() vitarusha rangi kwenye ndoo na kutengeneza rangi inayotakiwa. mashine.kichukuzi() tena itasogeza rangi mbali, na kisha rangi itaangaliwa kuona kama iko sawa. Unaweza kuandika programu ambayo itatengeneza aina zote tofauti za rangi?