TV ya Tvbot inaweza kuwashwa na kuzimwa kwa kutumia amri za "washa" na "zima". Jaribu.
Unaweza pia kubadilisha idhaa kwenye TV ya Tvbot. Unafanya hivyo kwa kuipa Tvbot amri ya "idhaa", na kuweka namba ya idhaa ndani ya mabano. Tvbot inaweza kurekebishwa kupata idhaa 0, 1, 2, 3, au 4.
Maroboti siyo vitu pekee kwenye Babylscript. Kuna vitu vingine ambavyo huwezi hata kuviona. Kuna kitu saa ambacho kinaweza kukupatia muda, lakini hakionekani kwenye skrini. Unaweza kutoa amri za "muda" na "tarehe" kwa saa kujua ni saa ngapi na siku gani.
Wakati mwingine unaweza kutoa amri moja kwa moja kwa kompyuta. Katika hali hii, huhitaji kuandika kitu (object) wala nukta. Andika amri tu. Mojawapo ya amri hizi ni "onesha". Amri ya onesha itaonesha namba kwenye skrini. Kama utaweka namba ndani ya mabano, namba hiyo itaoneshwa kwenye skrini.