KuanzaKutoa Amri kwa VituProgramu 1Programu 2KikokotoziVibadilikavyo: Kukumbuka VituMitungo 1Mitungo 2IngizoIkiwaWakati: Mizingo na Vitu VinavyojirudiaNamba Nasibu na ChaguaFSM: Mashine ya Hali Yenye Kikomo
Kutoa Amri kwa Vitu

Babylscript ni lugha ya uelekeo-kitu. Hiyo inamaanisha kwamba lugha hiyo ina vitu ambavyo unaweza kuvipa amri. Ni kama tu ilivyo katika maisha halisi. Kama una mbwa, unaweza kumwambia "akae" au "aviringike."

Kama ukiangalia kushoto, utaona maroboti wawili. Yule wa kushoto anaitwa zbot kwa sababu ana "Z" kubwa juu yake. Yule wa kulia anaitwa tvbot kwa sababu ana tv kubwa. Vyote Zbot na tvbot ni vitu. Unaweza kuvipa amri.

Kuvipa amri, unatakiwa kwanza upeleke puku yako ndani ya boksi la bluu la Eneo la Kuprogramu na kubofya.

Kisha, unaandika ni kwa nani unataka kutoa amri. Baada ya hapo, unaweka nukta. Kisha, unaandika ni amri gani unataka kutoa. Na kisha, unaandika mabano mawili na nukta-mkato (nukta-mkato ni alama ionekanayo kama mkato pamoja na nukta juu yake). Kwahiyo kama unataka zbot apunge mkono wake, ungeandika, "zbot.punga();" Hakikisha herufi zote ni ndogo. Babylscript itachanganyikiwa kama utatumia herufi kubwa.

Na mwisho, unatakiwa kubofya kitufe cha Endesha.

Endelea na jaribu kufanya zbot apunge. Kumbuka, hatua ni 1. bonyeza ndani ya boksi la bluu la Eneo la Kuprogramu, 2. andika "zbot.punga();", na kisha 3. bonyeza Endesha. Hakikisha unaandika vyote sahihi jinsi viliyvo.

Sasa, jaribu kumfanya tvbot apunge. Kwanza, bonyeza kitufe cha Safisha kuondoa amri ya zamani. Bonyeza ndiyo pale kompyuta itakapokuuliza kama unataka kusasfisha programu yako.

Kisha, ni kama awali ila badala ya kuandika zbot, andika tvbot. (Tvbot ana mikono midogo, kwahiyo hupunga kidogo tu.)

Zbot na tvbot wanajua kufanya vitu vingi. Hivi ni vitu unavyoweza kuwaambia wafanye: "mwekamweka," "pigamakofi," na "ruka." Tvbot hana miguu yoyote, kwahiyo hawezi kuruka. Jaribu hizi amri mbalimbali.

Kama utatoa amri kwa roboti mmoja wapo ambayo hataielewa, usiwe na wasiwasi. Ni kunguni, na Babylscript italalamika na kukuambia tatizo ni nini katika Eneo la Rangi ya chungwa la Taarifa.

Unaweza pia kuandika zaidi ya amri moja kwenye Eneo la Kuprogramu.

Kompyuta itafuata amri ya kwanza, na kisha kufanya amri inayofuata, na kisha inayofuata tena, mpaka itakapofika mwisho. Hii orodha ya maelekezo inaitwa "programu."

|

Programming Basics

Programming Basics: Beginners

Barua Pepe | Kuhusu | Sera ya Faragha